Page 40 - Quran inTakafitu
P. 40
UU I AL BAQARAH (2) AUF LAM MYM

108. je, (nyinyi makafiri wa umma huu);
Mnatakakumwuliza Mtume wenu kama
alivyoulizwa Musa zamani? Na anayehadilisha
Uislamu kwa ukafiri, hila shaka amepotea njia iliyo
sawa.

109. Wengi miongoni mwa watu waliopewa
Kitabu wanapenda wangekurudisheni nyinyi muwe
makafiri baada ya kuamini kwenu, kwa sabahu ya
husuda iliyomo nyoyoni mwao; (iJiyowapata) baada
ya kuwapambanukia haki. Basi (nyinyi Waislamu)
sameheni na puuzeni mpaka Mwenyezi Mungu alete
amri yake. Hakika Mwenyezi Mungu nj mwenye
uweza juu ya kila kitu.

110. Na simamisheni Bala na toeni Zaka; na
kheri nllakazozitanguliza, kwa ajm ya nafsi zenu,
mtazikuta kwa Mwenyezi Mungu. HakikaMwenyezi
Mungu anayaona (yote) mnayoyafanya.

111. Na walisema: "Hataingia Peponi ila aliye
Myahudi au Mkristo." Hayo ni matamanio yao tu
(si hukumu ya Mungu). Serna: "Leteni dalili zenu,
kama nyinyi ni wasc::rna kwelL"

"'

112. Naam, wanaoelekeza nyuso zao kwa
Mwenyezi Mungu, na wakawa ni watendaji mema
(kwa viumhe wellziwao), basi wao watapata malipo
yao kwa Mola wao, wala haitakuwa khofu juu yao
wala hawatahuzunika.

1 13. N a Mayahudi husema: "Wakristo hawana
cho chote Ccha m\ltegemeo katika dini yao)"; na
Wakristo husema: "Mayahudi hawana cho chote
Ccha rnategemeo katika dini yao)"; na hali wote
wanasoma Kitabu (walichoteremshiwa hila ya
kufuata yaliyomo ndani yake). Na hivi ndivyo wale
wasiojua Cmakafiri wa Kiarabu) wasemavyo. Ni
mfano wa kauli yao (wale waliopewa Vitabu. Kila
dini moja ininukana dini ya pili). Basi Mwenyezi
Mungu atahukumu baina yao siku ya Kiyama katika
yale waJiyokuwa wakikhitilafiana.

1 14. N a ni nani dhalimu mkubwa kuliko yule
anayezuia misikiti ya Mwenyezi Mungu kwamba
humo lisita;we jina lake na aka;itahidi kuiharibu?

Na tamko hili Iinashabihi tamko la Kiyahudi ambalo maana yake ni "Wewe mjinga mpolofu!' ,
Basi Mayahudi wakaona wamepata njia nzuri ya kumtukana Mtume kipunjo pasina mwenyewe kujua wala w.IU

wake kutambua. Ikawa wakifika barazani kwa Mtume hukithirisha kumwambia Mtume 'Raainaa'; na

wanakusudia maana ya 'Wewe mjinga mpotofu!'
Mwenyezi Mungu akakataza kutumiwa hilo lamko la Raainaa katika kumsemeza Mtume; Watumie'tamko

jengine lenye maana ile ile. Nalo 'Ndhurnaa;' na maana yake oi ile ile ya kuwa'Tutazame kamartlchungaji'
mwema anavyotazama wanyama wake"

25 5
   35   36   37   38   39   40   41   42   43   44   45