Page 38 - Quran inTakafitu
P. 38
UU I AL BAQARAH (2)

99. Hakika tumekuteremshia hoja zilizo wazi;
na hakuna wanaozikataa ila wale wanaovun;a amri
(ia Mwenyezi Mungu).

100. Oh~ kila mara wanapofunga' ahadi (hawa
Mayahudi), baadhi yao w(.naitupa? Bali wengi katika
wao hawaamini Cio lote).

101. Na walipojiwa (Mayahudi) na Mtume
kutoka kwa Mwenyezi Mungu, mwenye kusadikisha
yale yaliyo pamoia nao, (Naye ni Nabii
Muhammad), kundi moja miongoni mwa wale
waliopewa Kitabu (cha Mwenyezi Mungu­
TauratO lilitupa Kitabu cha Mwenyezi Mungu
(hicho) nyuma ya migongo yao kama kwamba
hawajui.

102. Wakafuata yale waliyoyafuata mashetani,
(wakadai kuwa yalikuwa) katika ufalme wa (Nabii)
Suleiman; na Suleiman hakukufuru, bali mashetani
ndio waliokufuru, wakiwafundisha watu uchawi
(waliokuwa wakiujua wenyewe tangu zamani), na
(uchawO ulioteremshwa kwa Malaika wawili, Haruta
na Maruta, katika (mji wa) Babil. Wala (Malaika
hao) hawakumfundisha yo yote mpaka wamwambie:
"Hakika sisi ni mtihani (wa' kutazamwa kutii
kwenu); basi usikufuru." Wakajifunza kwao ambayo
kwa mambo hayo waliweza kumfarikisha mtu na
mkewe (na mengineyo). Wala hawakuwa wenye
kumdhuru yo yote kwa hayo ila kwa idhini ya
Mwenyezi Mungu. Na wanajifunza ambayo
yatawadhuru wala hayatawafaa. Na kwa yakini
wana;ua kwamba aliyekhiari haya hatakuwa na
sehemu yo yote katika Akhera. Na bila shaka ni
kibaya kabisa walichouzia (starehe za) nafsi zao (za
Akhera). Laiti wangalijua, (hakika wasingefanya
hivi).

Sahihi za Mlume, kama Ibn Kalbir. Tazama Juzuu ya kwanza sahifa 124, hutaiona tafsiri hiyo. Wala Maimamu'

wa kUlaja hadithi sahihi za Mtume-na wakataja tafsiri ya Quran-hawa pia hawakuitaja tafsiri biyo; ila warnelaj.

kama walivyotaja Maimamu hawa; -Ibn jarir, Ibn Kathir, Ibnul Mundhir, Al Bayhaqy, Ibn Is-hact na Abu

Nunym, kama ilivyo katika sahifa 99 ya Fat-hul Qadyr ya Imam Ash Shaukany. Na ndivyo alivyofasiriImam Al

Bukhary, kp,ma ilivyo katika sahifa 124 ya Juzuu ya 8 ya Fat-hul Bary (Pamoja na kuisoma hiyo Fat-hul Bary).

Basi hiyo ya kuwa waliomba kwa jaha ya Mtume siyo NDIYO: ingawa imetajwa na Wafasiri wengi wa nyo~.

baada ya hao SALAF wa kutegemewa. .

Haikuja hadithi ya Mtume SAHIHI inayosema walU wamwombe Mwenyezi Mungu kwa jaha za viumbe Vyake

wala majina yao; wala haikusihi katika dua za Mtume dua ya kuomba kwa jaha za viumbe. .

Imekuja katika Qurani na Hadilhi Sahihi kuombwa Mwenyezi Mungu kwa majina Yake. Basi tufupizike na

Alivyotwambia Mwenyezi Mungu na Mtume Wake. WaIlahi hatutakuwa watovu kwa kufupizika juu ya haya.

Ama kuomba maiti badala ya kumwomba Mwenyezi Mungu - kama ilivyo katika Dua ya SAALTUKA"7 haya

yamcpindukia rnipaka-yametia maji maziwani.

93. Muradi ni kuwa walipewa amri lakini hawakuzifuata. Si kuwa walisema kwa mdomo "Tuna'sikia na

tunakataa. "

23
   33   34   35   36   37   38   39   40   41   42   43